Mayote

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mayotte)
Mayote
Départment de Mayotte (Kifaransa)
Flag of France Coat of Arms of Mayotte
(Bendera ya Mayote) (Nembo la Mayote)
Wimbo wa taifa: La Marseillaise
Mahali pa Mayotte
Lugha za Taifa Kiswahili (shimaore)
Kifaransa
Mji Mkuu Mamoudzou
Rais
Rais wa Ufaransa
Emmanuel Macron
Eneo
 - Jumla
 - 0.4% Maji
Kadiriwa 185 duniani
374 km²
Umma
 - Kadirio 2019 (270,372)
 - Sensa, julai 2002 (160,265)
 - Umma kugawa na Eneo (kilomita) 720
Kadiriwa 187 duniani
; (11 duni)
Chumo cha uchumi
 - Jumla
 - kwa kipimo cha umma
$466.8 billion (208 kadir)
$2,600 (165)
Uhuru
 - Kadirifu
 - Barabara
Eneo la Ufaransa
Kura ya maoni kubaki eneo la Ufaransa
Fedha Euro
Saa za Eneo UTC +3
Wimbo wa Taifa La Marseillaise
Intaneti TLD .yt
kodi za simu 269

Mayote ni eneo la ng’ambo la Ufaransa (kwa Kifaransa: Départment de Mayotte). Linaundwa na visiwa vya Maore na Pamanzi pamoja na vingine vidogo. Eneo hili kijiografia ni hasa muungo wa funguvisiwa la Komori lakini si kisiasa.

Ramani ya Komori na Mayote.

Mayote iko katika kaskazini ya Mfereji wa Msumbiji kwenye Bahari Hindi, kati ya Madagaska upande wa mashariki-kusini na Msumbiji bara upande wa magharibi. Iko kilometa 295 magharibi kwa Madagaska na km 67 kusini mashariki mwa Nzwani.

Ardhi ya Mayote ina eneo la takriban km² 374. Ni mwamba wa matumbawe.

Mji mkuu ni Mamoudzou tangu mwaka 1977. Mji mkuu wa zamani ni Dzaoudzi kwenye kisiwa cha Pamanzi.


Historia[hariri | hariri chanzo]

Andriantsoly, Sultani wa mwisho wa Mayote, 1832-1843.

Mayote inaonekana kuwa imekaliwa na watu kutoka karne ya 7, wakitokea Madagaska, wengine wenye asili ya Asia na wengine wenye asili ya Afrika.

Kati ya karne ya 8 na karne ya 11 wakazi walisilimu, na kuna msikiti mkongwe (katika Tsingoni) wa karne ya 14, pamoja na mirhab ya matumbawe (1532). Visiwa vyote vya Komori vinafuata utamaduni wa Kiswahili vikiwa pamoja na Mayote.

Mwaka wa 1841, wakati idadi ya watu ilipungua kwa wakazi chini ya 3000, sultani wa mwisho Andriansoly (kutoka Madagaska) aliuza kisiwa kwa Ufaransa kwa kubadilishana ya ulinzi wa nchi hiyo, hivyo Mayote ikawa koloni la Kifaransa.

Mwaka 1974, wakati visiwa vingine vitatu vya Komori walidai uhuru na kuunda Umoja wa Komori, Mayote iliomba kubaki na Ufaransa, na mwaka 2011 ilipewa hali ya eneo la ng'ambo la Ufaransa kwa kura ya maoni.

Lugha na dini[hariri | hariri chanzo]

Kuna lugha tatu ambazo huzungumzwa kisiwani Mayote, yaani Kifaransa (lugha rasmi), Kimaore ya Komori (55.1%), na Kibushi ya Madagaska.

Upande wa dini, asilimia 97 ni Waislamu na 3% ni Wakristo.

Utalii[hariri | hariri chanzo]

Kisiwa cha Mayote kina mchanga wa pwani ya rangi tofauti (nyeusi, kahawia, kijivu, nyekundu, beige, nyeupe). Rasi yake ni kubwa (km² 1500).

Usafiri[hariri | hariri chanzo]

Bahari karibu na Mamoudzou.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]


Nchi za Afrika Bara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira