(Translated by https://www.hiragana.jp/)
Adhana - Wikipedia, kamusi elezo huru Nenda kwa yaliyomo

Adhana

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mwadhini akialika waumini kutoka mnarani.
Sehemu ya mfululizo wa makala juu ya

Uislamu

Imani na ibada zake

Umoja wa Mungu
Manabii
Misahafu
Malaika
Uteule
Kiyama
Nguzo za Kiislamu
ShahadaSwalaSaumu
HijaZaka

Waislamu muhimu

Muhammad

Abu BakrAli
Ukoo wa Muhammad
Maswahaba wa Muhammad
Mitume na Manabii katika Uislamu

Maandiko na Sheria

Qur'anSunnahHadithi
Wasifu wa Muhammad
Sharia
Elimu ya Sheria za KiislamuKalam

Historia ya Uislamu

Historia
SunniShi'aKharijiyaRashidunUkhalifaMaimamu

Tamaduni za Kiislamu

ShuleMadrasa
TauhidiFalsafaMaadili
Sayansi
SanaaUjenziMiji
KalendaSikukuu
Wanawake
ViongoziSiasa
Uchumi
UmmaItikadi mpyaSufii

Tazama pia

Uislamu na dini nyingine
Hofu ya Uislamu

Adhana (neno hili asili yake ni Kiarabu أَذَان‎) ni wito maalumu wa kuwaita Waislamu kwenda kusali. Kwa kawaida Waislamu huwa na vipindi vitano vya ibada hasa katika sala za lazima (faradhi), hivyo wito huu hutumika kuwakumbusha waumini wa Kiislamu kwenda ibadani.

Lengo la adhana ni kuwajulisha watu kuwa muda wa ibada umefika na wakati mwingine hutumika kuwajulisha watu mahali nyumba ya ibada inapopatikana kwa wale wageni wa eneo husika.

Kitendo cha kutoa adhana huitwa kuadhini na mtu anayetoa adhana huitwa mwadhini.

Adhana hutolewa katika vipindi vya ibada yaani, alfajir, adhuhur, l-asr, magharib na l-ishaa.

Waislamu wote wanaitana hivyo katika sala zao:

  1. Allāhu Akbar (mara nne)
  2. Ašhadu an lā ilāh illā Allāh (mara mbili)
  3. Ašhadu anna Muḥammadan Rasūl Allāh (mara mbili)
  4. Ḥayya ʿalā al-salāt (mara mbili)
  5. Ḥayya ʿalā l-falāḥ (mara mbili)
  6. Allāhu Akbar (mara mbili)
  7. Lā ilāh illā Allāh (mara moja).
Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.