Shaba
Shaba au Kupri (cuprum) | |
---|---|
Jina la Elementi | Shaba au Kupri (cuprum) |
Alama | Cu |
Namba atomia | 29 |
Mfululizo safu | Metali |
Uzani atomia | 65.54 |
Valensi | 2, 8, 18, 1 |
Ugumu (Mohs) | {{{ugumu}}} |
Kiwango cha kuyeyuka | 1357.77 K (1084.62°C) |
Kiwango cha kuchemka | 2835 K (2562 °C) |
Asilimia za ganda la dunia | 0.01 % |
Hali maada | mango |
Shaba au shaba nyekundu (pia: Kupri au Cupri kama jina la kisayansi) ni elementi yenye namba atomia 29 kwenye mfumo radidia, uzani atomia ni 65.54. Alama yake ni Cu.
Katika mazingira ya kawaida ni metali yenye rangi ya kahawia nyekundu. Kiwango chake cha kuyeyuka ni 1,083 C°.
Ni kati ya metali za kwanza wanadamu walizotumia baada ya kutoka katika zama za mawe. Si metali ngumu sana, hivyo ilikuwa nyepesi kushughulikiwa na wanadamu wa kale.
Ikichanganywa na stani kunatokea aloi ya bronzi ambayo ni ngumu zaidi. Aloi nyingine ni shaba nyeupe, mchanganyo wa shaba nyekundu na zinki.
Wakati mwingine shaba hupatikana kama metali tupu lakini mara nyingi zaidi kama mtapo.
Tabia muhimu ya shaba ni uwezo wake wa kupitisha umeme. Hivyo imekuwa msingi wa teknolojia yote ya umeme hasa nyaya za kila aina.
Siku hizi shaba huchimbwa hasa katika nchi za Chile (Chuquicamata), Marekani, Urusi, Afrika ya Kati ("Copperbelt" - kanda la shaba), Congo-Zaire, Zambia, Kanada na Peru.
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Punje ndogo za shaba: shaba inaweza kutokea kwa rangi nyekundunyekundu; ikikaa hewani hubadilika kuwa na rangi ya machungwa mabivu
-
Kupri
-
Kupri