(Translated by https://www.hiragana.jp/)
Fyodor Dostoyevski - Wikipedia, kamusi elezo huru Nenda kwa yaliyomo

Fyodor Dostoyevski

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Fyodor Dostoyevski - uchoraji wa Vasily Perov 1872

Fyodor Mikhailovich Dostoyevski (Kirusi: Фёдор Миха́йлович Достое́вский) (11 Novemba 1821 (30 Oktoba ya Kalenda ya Juliasi) – 9 Februari 1881 (28 Januari ya kalenda ya kale) alikuwa mwandishi wa riwaya nchini Urusi. Mara nyingi ametajwa kama mwandishi Mrusi muhimu zaidi. Kati ya riwaya zake zianzojulikana kimataifa ni "Kosa na adhabu" pamoja na "Ndugu Karamasov".

Dostoyevski alizaliwa katika familia ya makabaila maskini babake alikuwa mganga. 1838-1843 alisoma uhandisi kwenye chuo kikuu cha kijeshi mjini Sankt Peterburg. 1839 alipata habari ya kwamba baba aliuawa na wakulima waasi alipokaa kwenye shamba lake. 1844 Fyodor alianza kutunga riwaya yake ya kwanza "Watu Maskini" iliyopokelewa vizuri na kuweka msingi wa kwanza kwa umaarufu wake.

1847 Dostoyevski alishiriki katika kundi la wanamapinduzi akakamatwa na kupewa adhabu ya kifo akasamehewa na Tsar Nikolai I na badala yake akapewa adhabu ya kufanya kazi nzito kwa muda wa miaka minne huko Siberia. Baadaye alipaswa kujiunga na jeshi hadi 1859.

Aliedndelea kuandika na riwaya ya kwanza iliyopokelewa pia kimataifa ilikuwa "Kosa na Adhabu" inayosimulia habari za mwanafunzi wa chuoni Rodion Raskolnikov anayekuwa mwuaji lakini baadaye anaanza kutambua dunia upya. Uwezo wa Dostoyevski wa kuonyesha roho na saikolojia ya watu ulionekana bora katika riwaya hii.

Kibinafsi Dostoyeski alipambana na hamu ya kucheza kamari iliyomsababisha kuwa na madeni makubwa.

Riwaya yake ya mwishi ilikuwa "Ndugu Karamasov" ambayo alishindwa kuimaliza. Alipoaga dunia watu wapato 60,000 walishiriki kwenye mazishi yake.

Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Fyodor Dostoyevski kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.