Heroes
Heroes | |
---|---|
Nembo ya Heroes | |
Aina | Maigizo Aksheni Shujaa mkuu |
Nchi inayotoka | Marekani |
Lugha | Kiingereza |
Ina misimu | 4 |
Ina sehemu | Los Angeles, California |
Utayarishaji | |
Watayarishaji wakuu |
Tim Kring Dennis Hammer Allan Arkush Greg Beeman Adam Armus Kay Foster Jim Chory Jesse Alexander Michael Green Jeph Loeb J.J. Philbin Aron Eli Coleite |
Mhariri | {{{Mhariri}}} |
Sehemu | Los Angeles, California |
Muda | makisio ni dk. 43 |
Urushaji wa matangazo | |
Kituo | NBC |
Inarushwa na | 25 Septemba 2006 - hadi leo |
Viungo vya nje |
Heroes ni kipindi cha Marekani kilichobuniwa na Tim Kring, kwenye stesheni ya NBC mnamo 25 Septemba 2006. Kipindi hiki kinaeleza jinsi wahusika wanajitambua kama wana vipawa mbalimbali na jinsi vipawa hivi vinavyoathiri maisha yao.
Misimu tatu imeshaonyeshwa na ya nne ilianza mnamo 21 Septemba 2009. Msimu wa kwanza ulivutia watazamaji milioni 14.3 nchini Marekani. Msimu wa pili wa Heroes ilivutia watazamaji milioni 13.1 nchini Marekani.[1]
Misimu
[hariri | hariri chanzo]Msimu wa kwanza
[hariri | hariri chanzo]Msimu wa kwanza ina vipindi 23 ambavyo vilionyeshwa kuanzia 25 Septemba 2006 hadi 21 Mei 2007.[2] Inatuonyesha jinsi kundi la binadamu wanavyotambua kuwa wana vipawa fulani. Mohinder Suresh, ambaye ni daktari na profesa, anafanya utafiti kuhusu watu hawa wenye vipawa. Wote wanajaribu kukabiliana na vipawa waliyonayo, wakijaribu kila mbinu kuzuia mlipuko wa bomu utakaotokea mjini New York City.
Msimu wa pili
[hariri | hariri chanzo]Ilianza 24 Septemba 2007. Ina jumla ya vipindi 11. Watu hawa wenye vipawa ("heroes") wanashirikiana na kuja pamoja ili kuzuia uenezaji wa virusi utakaouwa watu wote duniani.
Msimu wa tatu
[hariri | hariri chanzo]Ina vipindi 25 iliyoanza kuonyesha mnamo 22 Septemba 2008.[3] Inaanza pindi Nathan Petrelli karibu auwawe. Wafungwa wanapata nafasi ya kukimbia jela na "The Company" inawasaka. Pia, wanatafuta namna ya kuwafanya binadamu wa kawaida wapate vipawa.Sylar anatafuta wazazi wake wa ukweli. Mwishowe, Nathan anauliwa baada ya kupigana na Sylar. Matt anamsakanya Sylar ili asiwe na uwezo wa kuwanasa watu wenye vipawa.
Msimu wa nne
[hariri | hariri chanzo]Mnamo 4 Mei 2009, NBC walitangaza kuwa Heroes msimu wa nne itakuwa na vipindi 19.
Wahusika Wakuu
[hariri | hariri chanzo]- Hayden Panettiere ameigiza kama mwanafunzi wa shule ya upili aitwaye Claire Bennet.
- Jack Coleman ameigiza kama Noah Bennet, ambaye ni baba'ke Claire.
- Santiago Cabrera ameigiza kama Isaac Mendez - mwenye kipawa cha kuchora.
- Tawny Cypress ameigiza kama Simone Deveaux - msanii.
- Greg Grunberg ameigiza kama Matt Parkman - afisa wa polisi.
- Ali Larter ameigiza kama Niki Sanders.
- Leonard Roberts ameigiza kama D.L. Hawkins - mumewe Niki.
- Noah Gray-Cabey ameigiza kama Micah Sanders - mtoto wa Niki na D.L.
- Masi Oka ameigiza kama Hiro Nakamura.
- Adrian Pasdar ameigiza kama Nathan Petrelli.
- Sendhil Ramamurthy ameigiza kama Mohinder Suresh.
- Milo Ventimiglia ameigiza kama Peter Petrelli.
- Zachary Quinto ameigiza kama Sylar.
Mafanikio
[hariri | hariri chanzo]Msimu | Saa | Mwanzo wa msimu | Mwisho wa msimu | Mwaka | Watazamaji milioni |
Watazamaji + DVR | Watazamaji (BBC2) |
---|---|---|---|---|---|---|---|
1 | Monday 9:00 pm | 25 Septemba 2006 | 21 Mei 2007 | 2006–2007 | 13.86 | 14.30 | 3.91 |
2 | Monday 9:00 pm | 24 Septemba 2007 | 3 Desemba 2007 | 2007–2008 | 11.46 | 13.10 | 3.81 |
3 | Monday 9:00 pm | 22 Septemba 2008 | 27 Aprili 2009 | 2008–2009 | 7.61 | 9.27 | 3.26 |
4 | Monday 8:00 pm (2009) Monday 9:00 pm (2010) |
21 Septemba 2009 | - | 2009–2010 | 5.36^ | - | - |
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "NBC Renews Drama Series Chuck, Life and Heroes for 2008-09 Season", 2008-02-13. Retrieved on 2008-02-13.
- ↑ "Heroes: How to Stop an Exploding Man - TV.com". TV.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-03-30. Iliwekwa mnamo 2008-04-19.
- ↑ Adalian, Josef (2008-05-23). "NBC Revamps Fall Plans, Delays Series Launches". TVWeek.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-02-12. Iliwekwa mnamo 2008-09-18.