(Translated by https://www.hiragana.jp/)
J - Wikipedia, kamusi elezo huru Nenda kwa yaliyomo

J

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Alfabeti ya Kilatini
(kwa matumizi ya Kiswahili)
Aa Bb Cc ch Dd
Ee Ff Gg Hh Ii Jj
Kk Ll Mm Nn Oo Pp
Qq Rr Ss Tt Uu Vv
Ww Xx Yy Zz

J ni herufi ya 10 katika alfabeti ya Kilatini ambayo ni pia mwandiko wa Kiswahili cha kisasa. Asili yake ni Iota ya alfabeti ya Kigiriki.

Maana za J

[hariri | hariri chanzo]
  • katika fizikia J ni alama ya jouli ambayo ni kipimo cha SI cha nishati.

Historia ya alama J

[hariri | hariri chanzo]

Historia ya herufi J ni pamoja na I.

Kifinisia
Y (yad)
Kigiriki
Iota
Kietruski
I
Kilatini
I
Kilatini Kipya
J
Kilatini Karibu Zaidi
Jj
Kilatini I Kilatini I Kilatini J

Asili ya alama ni picha andishi iliyoonyesha mkono. Wafinisia walikuwa rahisihsa alama hiyo na kuiita kwa neno lao la mkono "yad" (au: yod). Wakaitumia kama alama ya sauti "y" na pia ya "i" ndefu. Wagiriki wakaipokea kama "Iota" na kurahisisha umbo lake zaidi hadi kuwa mstari tu. Wakaitumia kwa sauti ya "i".

Alama ikaendelea hivyo katika alfabeti za Waetruski na za Kilatini. Katika Kietruski ilimaanisha yote vokali ya "i" na konsonanti ya "y" na Waroma wakapokea vile katika Kilatini.

Katika Ulaya wa karne watu hasa Wajerumani walianza kuona haja ka kutofautisha kati ya sauti ya "i" na sauti ya "y" wakaanzisha kutofautisha kati ya "i" na "j" (kwa matamshi ya y). Lakini kwa muda mrefu hadi karne ya 19 mwandishi wa I na J haukufuata utaratibu uliokubaliwa.

Wasemaji wa lugha kama Kiingereza na Kifaransa walitumia "J" kwa sauti ya "j" jinsi ilivyoingia katika Kiswahili.