(Translated by https://www.hiragana.jp/)
Jimmy Wales - Wikipedia, kamusi elezo huru Nenda kwa yaliyomo

Jimmy Wales

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wales akizungumza katika mkutano wa Wikimania wa mwaka wa 2007.

Jimmy "Jimbo" Donal Wales (amezaliwa 7 Agosti 1966) ni mwanzilishi na ni rais wa sasa wa Wikimedia Foundation. Anafahamika zaidi kama mwanzilishi wa kamusi elezo huru ya Wikipedia. Kwa sasa anaishi mjini St. Petersburg, Florida.

Hapo awali aliunda kamusi elezo huru ya kwanza iliyojulikana kwa jina la Nupedia. Kisha akaanzisha mradi mpya wa Wikipedia, ambayo hapo mwanzo ilibidi uwe moja kati ya miradi ya Nupedia. Badala yake mradi mpya wa Wikipedia ukapata shauku zaidi ukaja kuwa miongoni mwa miradi mikubwa mtandaoni kama ulivyo leo hii.