Inka
Mandhari
(Elekezwa kutoka Mainka)
Inka ilikuwa cheo cha mfalme mkuu au Kaisari wa Dola la Inka katika Peru na nchi jirani. Jina latumiwa pia kwa taifa la Wainka.
Kati ya karne za 13 hadi 16 walitawala dola kubwa upande wa magharibi ya Amerika Kusini. Kutoka mwanzo wake katika milima ya Andes za Peru dola lilienea hadi Ekuador, Bolivia, Chile na sehemu za Argentina na Kolombia.
Dola la Inka liliharibika na Wahispania waliofika kuanzia mwaka 1531 waliokuwa na silaha za juu. Tar. 15 Novemba 1532 Wahispania chini ya Francisco Pizarro walimkamata Inka Atahualpa wakamwua tar. 29 Agosti 1533.
Inka wa mwisho Tupac Amaru aliuawa na Wahispania mwaka 1572.
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Inka kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |