Mavuno
Mavuno ni mchakato wa kuvuna au kukusanya mazao na matunda baada ya kulima. Neno linataja pia matokeo ya kazi hiyo kwa kusema: "tulikuwa na mavuno makubwa". Hii ni kwa kawaida kazi ya mkulima au mtu anayelima shamba au bustani.
Kwa maana pana zaidi neno mavuno linaweza kutaja pia tokeo la ufugaji au uvuvi.
Katika mazingira ambako watu wengi ni wakulima majira ya mavuno ni kipindi muhimu zaidi cha mwaka kwa sababu matokeo mazuri au mabaya ya mavuno yanaamulia hali ya maisha katika miezi inayokuja.
Katika jamii ya kimila jinsi ilivyokuwa kote duniani kabla ya enzi ya viwanda majira ya mavuno yalikuwa na desturi nyingi na kuathiri pia utamaduni na dini pamoja na ibada za pekee kwa ustawi wa mavuno kabla na shukrani za kusheherekea mavuno mema baadaye.
Siku hizi mashine zinaenea mahali popote na kuchukua sehemu kubwa ya kazi ya mavuno.
Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mavuno kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |