Mkoko
Mkoko | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mkoko magondi (Rhizophora mucronata)
| ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
Mikoko ni aina za miti au vichaka vinavyokua katika maji ya chumvi kwenye fuko za bahari za kanda za tropiki[1]. Miti hii inaainishwa katika jenasi tatu: Bruguiera, Ceriops na Rhizophora katika familia Rhizophoraceae. Pengine jina hili hutumika kwa Theobroma cacao lakini afadhali jina mkakao litumike kwa mti huu.
Takriban 1/3 ya pwani kwenye tropiki huwa na mikoko au miti ingine inayoweza kukua katika maji ya chumvi[2]. Msitu wa mikoko huitwa kapa au wangwa.
Mizizi ya mikoko inaweza kushika matope na hivyo husaidia kukinga pwani na kujenga visiwa.
Spishi za Afrika
[hariri | hariri chanzo]- Bruguiera gymnorhiza, Mchofi, Mkoko Wimbi, Mshinzi, Msindi, Msinzi au Mui (Black mangrove)
- Ceriops tagal, Mkandaa au Mkoko Mkandala (Indian mangrove)
- Rhizophora mangle, Mkoko Mwekundu Magharibi (Red mangrove)
- Rhizophora mucronata, Mkoko Magondi au Mkoko Mwekundu Mashariki (Asiatic mangrove)
Spishi za mabara mengine
[hariri | hariri chanzo]- Bruguiera cylindrica (Bakau putih)
- Bruguiera exaristata (Rib-fruited mangrove)
- Bruguiera hainesii (Haines's mangrove)
- Bruguiera parviflora (Small-flowered mangrove)
- Bruguiera sexangula (Upriver orange mangrove)
- Ceriops australis (Ceriops australis)
- Ceriops decandra (Ceriops decandra)
- Ceriops pseudodecandra (Ceriops pseudodecandra)
- Ceriops zippeliana (Ceriops zippeliana)
- Rhizophora apiculata (Tall-stilt mangrove)
- Rhizophora x harrisonii (Harrison's mangrove)
- Rhizophora racemosa (Rhizophora racemosa)
- Rhizophora samoensis (Samoan mangrove)
- Rhizophora stylosa (Spotted mangrove)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Mizizi ya mikoko
-
Mkoko kama chanzo cha kisiwa kidogo
-
Kapa ya mikoko magondi
-
Ua la mkoko magondi
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Hogarth, Peter J. (1999). The biology of mangroves Oxford University Press, Oxford.
- ↑ Morphological and physiological adaptations: Florida mangrove website. Retrieved on 2010 February 13.
Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkoko kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |