(Translated by https://www.hiragana.jp/)
Moshono - Wikipedia, kamusi elezo huru Nenda kwa yaliyomo

Moshono

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Moshono ni kata ya Jiji la Arusha katika Mkoa wa Arusha, Tanzania, yenye postikodi namba 23118.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 26,890 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 20,698 [2] walioishi humo.

Moshono kuna taasisi za elimu kama vile Shule ya St Jude na shule ya msingi Moshono.

Kuna biashara kadha wa kadha na upatikanaji wa chakula ni rahisi kutokana na kuwa na migahawa mingi, hasa stendi ya daladala.

  1. https://www.nbs.go.tz
  2. "Sensa ya 2012, Arusha - Arusha CC" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2016-03-03. Iliwekwa mnamo 2016-05-20.
Kata za Wilaya ya Arusha mjini - Tanzania

Baraa | Daraja II | Elerai | Engutoto | Kaloleni | Kati | Kimandolu | Lemara | Levolosi | Moivaro | Moshono | Muriet | Ngarenaro | Olasiti | Olmoti | Oloirien | Osunyai Jr | Sakina | Sekei | Sinoni | Sokon I | Sombetini | Terrat | Themi | Unga Ltd


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Arusha bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Moshono kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.