Mto Marne
Chanzo | Grand Est |
Mdomo | Seine 48°48′57″N 2°24′40″E / 48.81583°N 2.41111°E |
Urefu | 514 km |
Marne ni mto wa Ufaransa, tawimto upande wa kulia wa Seine katika eneo la mashariki na kusini ya Paris. Una urefu wa kilometre 514 (mi 319).[1] Mto ulizipatia jina lake wilaya za Haute-Marne, Marne, Seine-et-Marne, na Val-de-Marne.
Mto Marne unaanza katika platuu ya Langres, unatiririka kuelekea kaskazini, kisha unaelekea magharibi kati ya Saint-Dizier na Châlons-en-Champagne, na kuungana na Seine katika Charenton katika Paris. Katika kanda la Champagne sehemu ya maji huongozwa katika ziwa la kujengwa na binadamu la Lac du Der-Chantecoq, ili kudhibiti mtiririko wa maji. Kwa njia hiyo kiwango cha maji cha chini huzuiwa.[2]
Mto Marne ulikuwa eneo la mapigano mawili wakati wa Vita vya Kwanza vya Dunia. La kwanza Lilikuwa mgeuko wa Vita vya Kwanza vya Dunia katika mwaka wa 1914. La pili lilitokea miaka minne baadaye, katika mwaka wa 1918.
Katika karne ya 19 na 20, Marne ulipendeza wachoraji na wasanii wengi; miongoni mwao ni:
- Camille Corot
- Paulo Cézanne
- Camille Pissarro
- Henri Rousseau, dit "Le Douanier Rousseau"
- Albert Marquet
- Raoul Dufy
- André Dunoyer de Ségonzac
- [Louis Vuillermoz]
- Maurice Boitel
- Daniel du Janerand
Wilaya na miji iliyopitwa na mto huu
[hariri | hariri chanzo]- Haute-Marne (52): Chaumont, Saint-Dizier
- Marne (51): Châlons-en-Champagne, Épernay
- Aisne (02): Chateau-Thierry
- Seine-et-Marne (77): Meaux
- Seine-Saint-Denis (93): Neuilly-sur-Marne, noisy-le-Grand
- Val-de-Marne (94): Nogent-sur-Marne, Créteil, Charenton-le-Pont, Champigny-sur-Marne, Saint-Maur-des-Fossés, Joinville-le-Pont, Saint-Maurice
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "The Marne at the Sandre database" (kwa French).
{{cite web}}
: CS1 maint: unrecognized language (link) - ↑ "Apprivoiser la Marne" (kwa French). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2006-11-24. Iliwekwa mnamo 2006-06-02.
{{cite web}}
: CS1 maint: unrecognized language (link)
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu maeneo ya Ufaransa bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mto Marne kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |