Mto wa Nzoia
Mto wa Nzoia ni mto wa Kenya unaotoka Mlima Elgon na kuwa na urefu wa kilomita 257 (maili 160). Unatiririkia kusini na kisha magharibi hatimaye unaingia katika Ziwa Viktoria karibu na mji wa Port Victoria.
Mto huu ni muhimu kwa maeneo ya Magharibi mwa Kenya, ukipitia kwenye eneo linalokadiriwa kuwa na wakazi zaidi ya milioni 1.5. Maji yake hutumika kwa umwagiliaji wa mimea mwaka mzima, wakati mafuriko ya kila mwaka ya kuzunguka eneo amana ya Budalang'i husababisha mchanga unaochangia uzalishaji mzuri wa kilimo katika eneo hili.
Kwenye eneo la viwanda lililoko Webuye, mto huingiwa na uchafu mwingi unaotoka kwenye viwanda vya karatasi na sukari katika eneo hilo.
Mto huu una idadi kubwa ya maporomoko ya maji ya kuvutia, na unakisiwa kuwa na uwezo wa kuzalisha umeme unaotokana na maji.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu maeneo ya Kenya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mto wa Nzoia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |