Serapioni wa Thmuis
Serapioni wa Thmuis (300 hivi - Thmuis, 370 hivi), alikuwa askofu wa mji wa Thmuis (leo Tell el-Timai) nchini Misri na mwandishi wa Kikristo kwa lugha ya Kigiriki.
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu na babu wa Kanisa.
Sikukuu yake inaadhimishwa na Wakatoliki tarehe 21 Machi[1] au 7 Machi.
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Bado kijana, alikwenda kuishi jangwani kama mfuasi wa Antoni Mkuu, aliyemrithisha mojawapo kati ya majoho yake mawili ya ngozi ya kondoo.
Baadaye aliongoza monasteri, akawa askofu wa Thmuis kabla ya mwaka 339. Akishirikiana na patriarki Atanasi wa Aleksandria alipambana na Uario na kwa ajili hiyo mwaka 359 aliondolewa na Kaisari Kostansyo II jimbo lake.
Tunatunza hadi leo sehemu za barua tatu alizzoandikiwa na Apolinari wa Laodikea na hasa barua tano alizoandikiwa na Atanasi, ambazo kati yake nne zinafafanua imani katika umungu wa Roho Mtakatifu.
Serapioni anazungumziwa na Jeromu katika para ya 99 ya kitabu chake De viris illustribus, ambamo vinatajwa maandishi yake kadhaa: dhidi ya Wamani, juu ya Zaburi na barua walau 55 kwa watu mbalimbali. Kati yake vimetufikia tu kitabu dhidi ya Wamani na barua mbili, mbali ya sehemu kadhaa.
Jina lake limekuwa maarufu zaidi kwa Sakramentari iliyochapishwa mwishoni mwa karne ya 19 ambayo ni muhimu kwa liturujia. Lakini hakuna hakika kama alihusiana nayo.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
- Mababu wa Kanisa
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Maandishi
[hariri | hariri chanzo]- Athanase d'Alexandrie, Lettres à Sérapion (introduction et traduction française de Joseph Lebon des quatre lettres sur la divinité du Saint-Esprit), coll. Sources chrétiennes, Textes grecs n° 15, Paris, Éditions du Cerf, 1947 (Puis 2006)
- Robert Pierce Casey (éd.), Saint Serapion of Thmuis. Against the Manichees, Harvard Theological Studies 15, Harvard University Press, 1931
- Panteleimon E.E. Rodopoulos (éd.), The Sacramentary of Serapion of Thmuis, Thessalonique, 1967
- Bernard Outtier, André Louf, Michel van Parys, Claire-Agnès Zirnheld, Lucien Regnault (trad.), Lettres des Pères du désert Ammonas, Macaire, Arsène, Sérapion de Thmuis, Abbaye de Bellefontaine, Bégrolles-en-Mauges, 1985
- Patrologia Graeca, vol. 40, coll. 895-942
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Richard Klein, Serapion von Thmuis, In Biographisch-Bibliographisches Kirchenlexicon (BBKL, Band 9, Bautz, Herzberg 1995, ISBN 3-88309-058-1, Sp. 1404-1405
- Maxwell E. Johnson, The Prayers of Serapion of Thmuis: A Literary, Liturgical and Theological Analysis, Rome, Pontificio Istituto Orientale, 1995
- Klaus Fitschen, Serapion von Thmuis. Echte und unechte Schriften sowie die Zeugnisse des Athanasius und anderer, coll. Patristischen Texte und Studien 37, Walter de Gruyter, 1992
- Bernard Botte, "L'euchologe de Sérapion est-il authentique?", Oriens Christianus, vol. 48, 1964, p. 50-56
- Chisholm, Hugh, ed. (1911), Encyclopædia Britannica (11th ed.), Cambridge University Press, S.V. Serapion
- Dmitrijevskij, in Trudy (Journal of the Eccl. Acad. of Kiev, 1894), No. 2; separately (Kiev, 1894); reviewed by A. Falov, Xpiv-ch. Bvravriva, i. 207-213; cp. Byzant. Zeitschr. iv. I (1895), p. 193
- G. Wobbermin, in Harnack-Gebhardt, Texte u. Untersuch., new series, ii. 3 b (1899)
- P. Drews, "Über Wobbermins Altchristliche liturgische Stücke aus d. Kirche Ägyptens", in Zeitschr. f. Kirchen-Geschichte, xx. 4 (Oct. 1899, Jan. 1900)
- F.E. Brightman, "The sacramentary of Serapion of Thmuis", in Journal of Theological Studies, i. and ii. (Oct. 1899, Jan. 1900)
- John Wordsworth, Bishop Sarapion's Prayer-Book (London, SPCK, 1899)
- P. Batiffol, in Bulletin de lit. eccls., p. 69 sqq. (Toulouse, 1899)
- August Brinkmann, "Die Streitschrift des Serapion von Thmuis gegen die Manichäer", Sitzungsberichte der Königlichen Preussischen Akademie der Wissenschaften, Philologisch-historische Klasse, 1894, p. 479-491
- Alexander Globe, "Serapion of Thmuis as Witness to the Gospel Text Used by Origen in Caesarea", Novum Testamentum, vol. 26, fasc. 2 (avril 1984), p. 97-127
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |