(Translated by https://www.hiragana.jp/)
Ufugaji wa kuku - Wikipedia, kamusi elezo huru Nenda kwa yaliyomo

Ufugaji wa kuku

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kuku wenye siha.

Ufugaji wa kuku ni aina ya uvyazaji wa kale sana.

Kuku ni viumbehai aina ya ndege wasioweza kupaa kama baadhi ya ndege wengine.

Kuku wana faida kubwa katika maisha ya mwanadamu yeyote yule: kwanza wao na mayai yao ni chakula kwetu, pia wanaweza kutumika katika shughuli mbalimbali za biashara na kutupatia faida.

Kuku huhitaji joto la kawaida ili kuweza kukua vizuri, la sivyo ukuaji wao utakuwa duni na hata kuja kufa.

Wafugaji wa kuku wanatakiwa kuwa makini katika kuwapatia viumbe hawa huduma za msingi ili wasidhurike.

Vifaranga wazuri waliotumiwa njia za kufaa.

Vifaranga ni vitoto vya tetea. Ufugaji wa vifaranga unaweza kuwa na faida au hasara. Humu tutaelezea njia za kupata vifaranga wazuri .

Kwa nini kuwa na vifaranga wengi wa umri mmoja?

[hariri | hariri chanzo]

1. Kutunza kuku kitaalam kwa urahisi.

2. Kupata mayai mengi kwa wakati mmoja.

3. Kuuza kuku wengi kwa wakati mmoja n.k.

Sifa za tetea wa kuatamia

[hariri | hariri chanzo]

1. Kuku mwenye umbo kubwa

2. Mwenye historia nzuri ya kuhatamia na hatimaye kutotoa vifaranga.

Sifa za mayai ya kuatamisha

[hariri | hariri chanzo]

1. Yasiwe machafu wala yasiwe na nyufa.

2. Yasiwe makubwa sana au ya duara, yasiwe na uvimbe.

Chumba cha kuatamia

[hariri | hariri chanzo]

1. Kuku wanaohatamia watengwe katika chumba ili kuondoa tatizo la kutagiana.

2. Mlango na dirisha yawekwe wavu ili muda wa mchana mwanga na hewa viweze kuingia ndani.

3. Chumba kiwe na nafasi ya kutosha ya kuweka viota, chakula na maji

Chakula na maji

[hariri | hariri chanzo]

Kuku wanaohatamia wapewe chakula cha kuku wakubwa wanaotaga cha kutosha muda wote kiwemo kwa kuwa kuku hawa hutoka wakati tofauti pia majani, mboga-mboga na maji ya kunywa ni muhimu sana. Vyote hivi viwekwe kwenye chumba ambacho kuku wanahatamia ili kumfanya kuku asiende umbali mrefu kutafuta chakula pia kuyaacha mayai kwa muda mrefu.

Changamoto za kuku wanaoatamia

[hariri | hariri chanzo]

1. Huhitaji sehemu kubwa kwa sababu, ili upate vifaranga wengi, unahitaji kuku wengi wanaotamia.

2. Kuwepo kwa wadudu kama utitiri na kutopatikana kwa chakula cha kutosha husababisha kuku kutoka toka nje na kwenda mbali na kusababisha mayai kuharibika.

3. Kuku kupata magonjwa wakati wanapotamia.

4. Kutokuwa na kipimo cha kupimia mayai yaliyo na mbegu.

Ukizingatia mambo haya utapata vifaranga wazuri wa kufuga na hata wa kuuza.

Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ufugaji wa kuku kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.