Urujuanimno
Urujuanimno (pia ultravaoleti, kwa Kiingereza: ultraviolet, kifupi: UV) ni aina ya nuru isiyoonekana na binadamu ila na wanyama mbalimbali. Kwa lugha nyingine na makini zaidi ni sehemu ya mnururisho wa sumakuumeme wenye lukoka (wavelength) baina ya nanomita 400 hadi 10, ambayo ni lukoka fupi kuliko urujuani inayoonekana lakini ndefu kuliko eksirei.
Wanyama wengi pamoja na wadudu kadhaa, mamba, ndege wengine wadogo wanaweza kutambua urujuanimno. Mnururisho wa urujuanimno unafika duniani kama sehemu ya nuru ya jua.
Mnururisho wa urujuanimno na afya ya watu
[hariri | hariri chanzo]Viwango vikubwa vya mnururisho wa urujuanimno vinaweza kusababisha uharibifu kwa seli za binadamu. Ngozi ya binadamu inajenga rangi ya melanini kama kinga dhidi yake. Tabaka la ozoni katika angahewa ya Dunia inachuja sehemu ya mnururisho huo lakini kwenye maeneo ya ikweta kiwango kinachofika hadi uso wa dunia ni kikubwa zaidi.
Ndiyo sababu ya kwamba watu katika maeneo karibu na ikweta wana rangi nyeusi zaidi. Watu wanaoishi mbali na ikweta hawahitaji kiwango hicho cha kinga dhidi ya mnururisho wa urujuanimno na kwa sababu hiyo watu wenye rangi nyeupe zaidi waliweza kuendelea huko kaskazini. Pale ambako watu kutoka sehemu za kaskazini walihamia katika maeneo ya ikweta wana hatari kubwa zaidi ya kupata kansa ya ngozi na hii inaonekana katika asilimia kubwa ya kansa hiyo kati ya Wazungu wa Australia.
Asilimia kubwa ya kansa ya ngozi kati ya watu walioathiriwa na uzeruzeru katika Afrika ina sababu hiyohiyo.
Uga sumaku ya Dunia hukengeusha kiasi kikubwa cha mnururisho wa urujuanimno pamoja na upepo Jua kutoka angahewa na kwa njia hiyo inakinga angahewa yetu.
Kujisomea
[hariri | hariri chanzo]- Hu, S; Ma, F; Collado-Mesa, F; Kirsner, R. S. (Julai 2004). "UV radiation, latitude, and melanoma in US Hispanics and blacks". Arch. Dermatol. 140 (7): 819–824. doi:10.1001/archderm.140.7.819. PMID 15262692.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - Hockberger, Philip E. (2002). "A History of Ultraviolet Photobiology for Humans, Animals and Microorganisms" (– Scholar search). Photochemisty and Photobiology. 76 (6): 561–569. doi:10.1562/0031-8655(2002)076<0561:AHOUPF>2.0.CO;2. PMID 12511035.
{{cite journal}}
: External link in
(help)|format=
- Allen, Jeannie (6 Septemba 2001). Ultraviolet Radiation: How it Affects Life on Earth. Earth Observatory. NASA, USA.
{{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Ultraviolet light from our sun (NASA) Archived 27 Januari 2011 at the Wayback Machine.
- What is ultraviolet light?
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Urujuanimno kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |