Ukanoni
Mandhari
(Elekezwa kutoka Wakanoni)
Ukanoni ni mtindo wa maisha ya kitawa katika kanisa katoliki uliokusudiwa hasa kwa mapadri wa parokia za mjini.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Ili kuboresha maisha ya mapadri wanajimbo, toka zamani ulisisitizwa uundaji wa jumuia kati yao, ambamo wasali na kufanya utume kwa pamoja.
Hasa kuanzia karne XI wengi walifanya hivyo kwenye makanisa makubwa kama mtindo mpya wa kitawa unaosisitiza liturujia ya fahari pamoja na uchungaji.
Inavyoweza kueleweka, hao walifuata kanuni ya Agostino wa Hippo na kuitwa Wakanoni. Maarufu zaidi katika yao ni Norbert (1082-1134), mwanzilishi wa Wapremontree.
Leo mtindo huo unaendelea katika mashirika mbalimbali, ambayo lakini hayana watu wengi kama aina nyingine za utawa.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Hugh of St. Victor. Explanation of the Rule of St. Augustine, (translated by Dom Aloysius Smith C.R.L.), Sands & Company, London, 1911 Archived 4 Oktoba 2013 at the Wayback Machine.
- Houses and Congregations C.R.S.A. Archived 12 Oktoba 2013 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |