Baisikeli
Baisikeli (kwa kawaida baiskeli; pia basikeli; kutoka Kilatini "bis", "mara mbili" na Kigiriki "κύκλος", kyuklos, "duara" kupitia Kifaransa/Kiingereza "bicycle") ni chombo cha usafiri kinachoendeshwa kwa nguvu ya misuli ya binadamu.
Baisikeli huwa na magurudumu mawili yanayoshikwa na fremu, kiti kimoja, kanyagio, breki na usukani. Tabia nyingine za kawaida ni kuwa na taa mbele na nyuma. Baisikeli bora huwa pia na gia zinazorahisisha kazi ya kukanyaga kanyagio.
Kwa kawaida nguvu hupelekwa kwa nyororo kutoka kanyagio kwenda gurudumu la nyuma. Magurudumu huwa na matairi yaliyojaa hewa.
Katika nchi nyingi baisikeli ni chombo muhimu cha usafiri. Zamani baisikeli ilikuwa usafiri wa maskini lakini pia katika nchi kadhaa zilizoendelea watu hutumia baisikeli ama kwa usafiri wa mjini au kwa burudani.
Sayansi imegundua ya kwamba baisikeli ni usafiri wa haraka mjini katika umbali wa kilomita chache. Katika nchi nyingi kuna njia za pekee kwa ajili ya baisikeli kando ya barabara ya magari.
Baisikeli ni usafiri unaotumia nishati kidogo na hivyo kuwa nafuu kwa hifadhi ya mazingira.
Mashindano ya baisikeli ni tawi muhimu la michezo ya kimataifa.
Baisikeli ya magurudumu matatu
[hariri | hariri chanzo]Aina ya pekee ya baiskeli hutengenezwa kwa magurudumu matatu (kwa Kiingereza tricycle). Mara nyingi kuna gurudumu moja mbele sawa na baisikeli ya kawaida na magurudumu mawili nyuma, lakini muundo wa kinyume hutumiwa pia.
- baisikeli za watoto na watu wenye matatizo (kama wazee) ya kuendesha baisikeli ya kawaida huwa na magurudumu matatu kwa sababu si rahisi kuanguka.
- baisikeli za kubeba mizigo au abiria hutengenezwa mara nyingi kwa magurudumu matatu maana ni thabiti zaidi.
Hivyo magari ya kubeba abiria aina ya riksha yaliendelezwa kuwa riksha ya baisikeli iliyoendelea kuwa mtangulizi wa bajaji.
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Usalama kwa watoto
-
Mwuza magazeti
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |