Jeff Agoos
Jinsia | mume |
---|---|
Nchi ya uraia | Marekani |
Nchi anayoitumikia | Marekani |
Jina halisi | Jeff |
Jina la familia | Agoos |
Nickname | Goose |
Tarehe ya kuzaliwa | 2 Mei 1968 |
Mahali alipozaliwa | Geneva |
Kazi | association football player, futsal player, sports executive |
Nafasi anayocheza kwenye timu | Beki |
Alisoma | University of Virginia, J. J. Pearce High School |
Muda wa kazi | 1994 |
Work period (end) | 2004 |
Mchezo | mpira wa miguu |
Ameshiriki | 2000 Summer Olympics, 2002 FIFA World Cup, 1998 FIFA World Cup |
Ligi | Major League Soccer |
Jeff "Goose" Agoos | ||
Maelezo binafsi | ||
---|---|---|
Jina kamili | Jeffrey Alan Agoos | |
Tarehe ya kuzaliwa | 2 Mei 1968 | |
Mahala pa kuzaliwa | Geneva, Uswisi | |
Urefu | 1.78m | |
Nafasi anayochezea | Difenda | |
Maelezo ya klabu | ||
Klabu ya sasa | Amestaafu | |
Klabu za vijana | ||
1986, 1988–1990 | Chuo Kikuu cha Virginia | |
Klabu za ukubwani | ||
Miaka | Klabu | |
1991 1991–1992 1994–1995 1996–2000 2000 2001–2004 2005 |
Maryland Bays Dallas Sidekicks SV Wehen DC United → West Bromwich Albion (mpango wa mkopo) San Jose Earthquakes MetroStars | |
Timu ya taifa | ||
1988–2003 | Ilikuwa Marekani | |
* Magoli alioshinda |
Jeffrey Alan "Jeff" Agoos (alizaliwa Geneva, Uswisi, 2 Mei 1968), ni mchezaji wa zamani wa Marekani, aliyecheza kama mlinzi. Ni mmoja wa wachezaji waliocheza mechi nyingi sana katika timu ya taifa ya Marekani.
Agoos (alipewa jina la utani la Goose), alizaliwa Uswisi, wakati baba yake alikuwa akifanya kazi huko. Hata hivyo, alilelewa katika eneo la Texas, na alishinda mataji matano ya Ligi Kuu ya Soka ya Marekani:tatu na D.C. United na mbili akiwa na San Jose Earthquakes. Yeye ,pia, alishinda Kombe la Marekani la 1996 na alikuwa difenda bora kabisa katika Ligi Kuu ya Soka ya Marekani katika msimu wa 2001. Alichaguliwa kuwa mmojawapo wa watu waliorodheshwa katika Ukumbi wa Taifa wa Umaarufu katika Soka katika mwaka wa 2009.
Wasifu
[hariri | hariri chanzo]Shule ya Upili
[hariri | hariri chanzo]Agoos alihudhuria Shule ya Upili ya J.J. Pearce katika eneo la Richardson, Texas. Alichaguliwa mara mbili na gazeti la Parade kama Mwanaspoti Bora Amerika wa shule ya upili na vilevile Mwanaspoti bora wa mwaka katika eneo la Dallas. Aliongoza timu yake kwenye michuano ya Jimbo la Texas katika mwaka wa 1983. Wakati wa majira ya joto ya 1985, Agoos alichaguliwa kuwakilisha Marekani katika michezo ya Maccabiah ya 1985.
Wasifu wa chuo kikuu
[hariri | hariri chanzo]Kutoka 1986-1990, Agoos alichezea soka timu ya Bruce Arena katika Chuo Kikuu cha Virginia. Katika misimu minne akiwa na Caveliers,akashinda tuzo ya Mwamerika Bora mara mbili,1988 na 1990. Yeye alimaliza akiwa # 2 katika uchaguzi wa Tuzo ya Hermann.
Katika mwaka wa 1989,Chuo Kikuu cha Virginia iliendelea na kufuzu katika Shindano la NCAA ambapo ilishindana na Chuo Kikuu cha Santa Clara na mechi ikaisha 1-1 baada ya muda wa ziada. Timu zote mbili zilitaka kuendelea kucheza lakini , afisa wa NCAA walimaliza mechi na wakasema timu zote mbili ndizo mabingwa. Wakati huo, hakukuwa na mikwaju ya penalti kutumika kumaliza mechi. Mwishoni mwa msimu, Agoos aliwakilisha Marekani wakati wa michezo ya 1989 ya Maccabiah.
Wasifu wa Hapo awali
[hariri | hariri chanzo]Alipofuzu kutoka chuo kikuu,Agoos alichezea timu ya Maryland Bays katika ligi ya A-League katika mwaka wa 1991. Tarehe 13 Februari 1991, timu ya Dallas Sidekicks ilimtaka Agoos katika orodha ya uchaguzi wa wachezaji ya jumla ya 1999. Katika mwaka wa 1992, yeye aliacha kuchezea Sidekicks ili kuchezea timu ya taifa ya Marekani kabisa.Ingawaje, timu ya Dallas ilimchagua tena katika orodha ya wachezaji.Wakati huu hakutia saini mkataba na timu hiyo.
Kuhamia Ujerumani
[hariri | hariri chanzo]Baada ya kutoka katika timu ya Marekani ya Shindano la Kombe la Dunia la 1994,Agoos akahamia Ujerumani kuchezea timu ya SV Wehen katika msimu wa 1994-95.
Ligi Kuu ya Soka ya Marekani
[hariri | hariri chanzo]Baada ya kurudi kutoka Ujerumani katika mwaka wa 1995, yeye alitumika kama kocha msaidizi kwa Bruce Arena katika Chuo Kikuu cha Virginia.
Katika mwaka wa 1996, Agoos alirejea Marekani ili kujiunga na Ligi Kuu ya Soka ya Marekani. Ili kuunda ligi, Ligi Kuu ya Soka ya Marekani ilwaweka wachezaji mbalimbali waliojulikana kwa kila timu. Katika kupangwa huku,Agoos aliwekwa D.C. United alipokutana na Bruce Arena ,kocha wa kwanza wa timu. Mwaka huo, Agoos alishinda na timu yake Ligi Kuu ya Soka ya Marekani na vilevile Kombe la Marekani. Mwaka uliofuata walishinda ligi tena. Katika mwaka wa 1998, DC United ilifanikiwa kabisa iliposhinda Vasco da Gama na kushinda Kombe la Amerika yote na wakashinda Ligi Kuu ya Soka ya Marekani kwa mara ya tatu. Katika miaka ya 2001 hadi 2004,alikuwa na San Jose Earthquakes na akaendelea na kushinda Ligi Kuu ya Soka ya Marekani yake ya nne na ya tano.
Agoos alituzwa kama difenda wa mwaka wa Ligi Kuu ya Soka ya Marekani katika mwaka wa 2001 na akapata nafasi katika timu bora ya Ligi Kuu ya Soka ya Marekani mara tatu(1997,1999 na 2001). Mwaka wa 2005,Agoos aliteuliwa katika mwaka wa kumi wa Ligi Kuu ya Soka ya Marekani katika timu bora ya wakati wote tangu ligi ianze.
Huduma zake ziliuziwa MetroStars baada ya msimu wa 2004 katika orodha ya daraja la nne ya wachezaji. Katika miaka kumi katika Ligi Kuu ya Soka ya Marekani, Agoos alifunga mabao 11 katika msimu na kusaidia katika kufunga mabao 25 katika mechi 244. Katika mwaka wa 2005, aliorodheshwa katika Wachezaji 11 bora wa Ligi Kuu ya Soka ya Marekani kabla ya kustaafu 8 Desemba 2005.
Timu ya taifa
[hariri | hariri chanzo]Agoos alichezea timu ya taifa kwa mara ya kwanza mnamo 13 Januari 1988 dhidi ya Guatemala. Alikuwa mchezaji wa mwisho wa timu kutolewa kwa kikosi cha Marekani cha kucheza katika Shindano la Kombe la Dunia la 1994 ,alichoma sare yake alipopata habari hii. Yeye alikuwa katika kikosi cha Shindano la Kombe la Dunia la 1998 nchini Ufaransa lakini hakucheza hata dakika moja huku David Regis akichaguliwa. Shindano la Kombe la Dunia la 2002 nchini Korea Kusini,(akiwa umri wa miaka 34)alicheza mechi tatu na akajifunga bao katika ushindi wao dhidi ya Ureno. Aliuumia hapo baadaye n katika mechi dhidi ya Poland. Hivyo basi,hakucheza tena katika shindano hilo. Alicheza mara 134 kwa jumla katika timu ya taifa ya Marekani,mechi yake ya mwisho ilikuwa dhidi ya Wales hapo 26 Mei 2003.
Agoos alikuwa katika timu ya Marekani ya Futsal ya 1992 iliyoshinda medali ya fedha Hong Kong. Alichezea timu hiyo mara 10 na akafunga mabao 2 akiwa timu hiyo.
Baada ya kustaafu
[hariri | hariri chanzo]Agoos aliajiriwa kama Mkurugenzi wa Kitaalam wa New York Red Bulls mnamo Tarehe 28 Septemba 2006 akifanya kazi chini ya kocha mkuu Bruce Arena. pia alijiunga rasmi na shirika la Bulls mnamo tarehe 1 Januari 2007. [15] Tarehe 7 Januari 2008, alipandishwa cheo kuwa Mkurugenzi wa Michezo.
Katika mwaka wa 2009,Agoos aliorodheshwa katika Ukumbi wa Taifa Umaarufu katika Soka.
Tuzo
[hariri | hariri chanzo]Marekani
[hariri | hariri chanzo]- Kombe la dhahabu la CONCACAF (1): Kombe la dhahabu la CONCACAF la 2002
D.C. United
[hariri | hariri chanzo]- Kombe la Ligi Kuu ya Soka ya Marekani - Washindi (3): 1996, 1997, 1999
- Ngao ya Ligi Kuu ya Soka ya Marekani - Washindi (2): 1997, 1999
- Kombe la Marekani - Washindi (1): 1996
- Kombe la CONCACAF la Kombe la Mabingwa - Washindi (1): 1998
- Kombe la Amerika - Washindi (1): 1998
San Jose Earthquakes
[hariri | hariri chanzo]- Ligi Kuu ya Soka ya Marekani- Washindi(2): 2001, 2003
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- http://www.ussoccerplayers.com/players/alumni/index.html?player_id=2
- http://www.jewishvirtuallibrary.org/jsource/biography/Jeff_Agoos.html
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Jeff Agoos kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |