(Translated by https://www.hiragana.jp/)
Natanaeli wa Kana - Wikipedia, kamusi elezo huru Nenda kwa yaliyomo

Natanaeli wa Kana

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Natanaeli wa Kana katika dirisha la kioo cha rangi.

Natanaeli kutoka Kana ya Galilaya ni mfuasi wa Yesu Kristo ambaye aliletwa kwake mapema na rafiki yake, Mtume Filipo, akaondolewa wasiwasi akamkiri Yesu kuwa Mwana wa Mungu, Mfalme wa Israeli (Injili ya Yohane 1:45-50).

Baada ya ufufuko wa Yesu, anatajwa tena (Yoh. 21:2) kuwa mmoja kati ya wanafunzi waliomfuata Mtume Petro kwenda ziwani kuvua samaki.

Wengi wanaona ni yuleyule ambaye katika Injili Ndugu anaitwa Bartolomayo, yaani mwana wa Tolomayo.

Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Natanaeli wa Kana kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.